Kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya
FIFA wa timu ya taifa ya
Tanzania Taifa Stars dhidi ya
Botswana September 2 uwanja wa
Uhuru Dar es Salaam, wachezaji wa kimataifa wa
Tanzania walioitwa wengi tayari wameungana na wenzao.

Simon Msuva
Miongoni mwa wachezaji waliyoitwa
Taifa Stars ni
Simon Msuva anayecheza
Difaa El Jadid ya
Morocco na
Farid Musa anayecheza
Tenerife ya
Hispania lakini vipi mbona hatuwaoni na wenzao, ukilinganisha wenzao wa nje
Abdi Banda,
Mbwana Samatta na
Elias Maguli wameshawasili?
Kocha mkuu wa
Taifa Stars Salum Mayanga amezungumzia kuhusiana na ishu hiyo
“Namshukuru
Mungu vijana wako salama lakini kuna wachezaji wawili bado hawajafika,
Msuva alikuwa na tatizo la visa ilikwisha kule, hivyo tulilazimika
kubadilisha mara tatu tiketi yake kule, lakini hadi saa tano asubuhi leo
kulikuwa na uwezekano wa kuanza safari”

Farid Musa
“Kuhusu Farid tayari yupo kambini amefika jioni hii
lakini amepumzika kutokana na safari ndefu lakini Monreal anayecheza
Ureno ndio tunadhani mtu pekee ambaye hatohudhuria mechi hii, kwa kiasi
kikubwa asilimia 90 wachezaji wote wapo”
Source : millard Ayo
No comments:
Post a Comment