Mastaa wa soka wa
Man City Kyle Walker na
John Stones ambao wanalipwa mishahara mikubwa ndani ya
Man City leo wameonekana wakienda mazoezini na gari ndogo, thamani yake inatajwa kufikia pound 5000 ambazo ni zaidi ya milioni 14.

Kyler Walker
Kyler Walker analipwa mshahara wa pound 130000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 370 wakati
John Stones analipwa mshahara wa pound 100000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 288,
Stones na
Walker leo wameonekana wakitembelea gari yenye gharama ndogo.

Licha ya mastaa hao kuwa na uwezo wa kumiliki gari aina yoyote ambayo mioyo yao itapenda kutumia,
John Stones alionekana akimuendesha
Kyler Walker
katika gari hiyo na kuelekea mazoezini wakiwa wanafuraha, kitendo hicho
kimewafanya waingie kwenye headlines kwa sababu haijazoeleka kuona
mastaa kama wao kutembelea gari za bei ndogo.

John Stones
Kwa pamoja
Walker na
Stones
wanalipwa pound 230,000/= ambazo ni zaidi ya milioni 650 za kitanzania,
mshahara ambao kila mmoja anaweza kununua aina yoyote ya gari, sema
wameamua kutembelea gari ya kawaida.
No comments:
Post a Comment