LICHA ya kusambaa video yake ya zamani
akielezea anavyompenda msanii wa Bongo Fleva, Barakah The Prince huku
akionesha tattoo aliyojichora jina lake, staa wa sinema za Kibongo,
Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kufunguka kuwa mpenzi wake wa sasa
hafurukuti kwani anamwamini vilivyo.
Nisha.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nisha
alisema kuwa, licha ya watu kutaka kumuharibia kwa mpenzi wake huyo
aliyemtaja kwa jina moja la Minu kwa kurusha mitandaoni video za wapenzi
wa zamani, hawawezi kumuachanisha naye kwa sababu mwanaume wake huyo
anamwamini. “Hiyo video ya Barakah ni ya zamani
sana, lakini ninaona watu wameiweka ili waniharibie kwa Minu, jambo
ambalo haliwezekani kwani ananiamini na yuko peke yake kwangu, nami niko
peke yangu kwake,” alisema Nisha.
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment