RAPA wa kike anayefanya vizuri kwenye Hip Hop Bongo, Claudia Lubao
‘Chemical’, amefunguka kuwa, msanii Stereo ambaye amekuwa akijanasibu
kwenye vyombo vya habari kwamba anampenda, ukweli ni kwamba mwanamuziki
huyo hajawahi kumpenda
kwa dhati kwa kuwa bado mwanaume huyo hajamwonesha vitendo vyenye kuthibitisha hilo.

Stereo.
Akipiga stori na Showbiz Extra, Chemical alisema kuwa, hajawahi kupendwa kwa dhati na Stereo
kwa kuwa hata siku moja, hajawahi kuelezwa kitu chochote kinachohusu
mapenzi na rapa huyo, zaidi ya kumsikia tu kwenye vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii.
“Siwezi kujiongopea kwamba nimewahi kupendwa na Stereo, hata mara
moja rapa huyo hajawahi kunipenda, nasema hivyo kwa sababu hajawahi
kunifungukia live, ninaishia kumsikia tu kwenye media na mitandao ya
kijamii,” alisema Chemical.
No comments:
Post a Comment