Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Serikali haikatazi
Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya dawa lakini ni vizuri wakazingatia
kuweka maduka hayo mbali na Vituo vya Afya vya Serikali na Hospitali ili
kusiwe na aina yoyote ya kutanguliza maslahi yao kwanza katika kutoa
huduma za dawa kwa wagonjwa.Ameeleza kuwa kwa sasa Serikali imejitahidi kuongeza upatikanaji wa dawa na imeamua kuanza kununua dawa kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa awali.
>>>”Watendaji badala ya kuwaandikia wagonjwa dawa zilizo kwenye orodha, wanaandika dawa zao na kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa kwenye maduka ya dawa. Hatukatazi Watumishi kuwa na maduka ya dawa ila muhimu kuchora mstari wa dawa za Serikali na dawa ambazo sio za Serikali.” – Waziri Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment