Mourinho asubuhi ya leo saa nne tayari alikuwa amewasili katika mahakama mjini Madrid katika eneo liitwalo Puzuelo Del Alacron tayari kusikiliza hukumu ya kosa hilo alilotenda wakiwa akiwa Real Madrid.
Baada
ya muda kesi hiyo kuisha Mourinho alitoka nje ya mahakama ambako
kulikuwa na waandishi wa habari na kuwaambia kuwa amekubali kulipa kiasi
hicho anachodaiwa ambapo ni €3.3m.Kesi ya Jose Mourinho ilikuwepo tangu mwezi wa sita mwaka huu akidaiwa kwamba alikuwa akikwepa baadhi ya masuala ya kodi katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2013.
Wakati
kesi ya Mourinho inaanza alikana mashtaka na kusema aliondoka Hispania
akiwa msafi kuhusu kodi na wakili wake aitwaye Gestifute Media
akizishangaa mamlaka za kodi za Hispania akidai Mourinho alilipa zaidi
ya £23m ya kodi akiwa Hispania.Hii sio mara ya kwanza kwa wanasoka katika ligi kuu La Liga kukumbwa na kashfa za ukwepaji kodi kwani Angel Di Maria, Lioneil Messi, Cristiano Ronaldo na Javier Mascherano wameshakumbwa na kesi za namna hii.
Baada ya kesi hiyo sasa Mourinho anapakia ndege kurudi nchini Uingereza kuiandaa timu kwa ajili ya pambano kubwa na gumu siku ya Jumapili zidi ya Chelsea

No comments:
Post a Comment