Malaika Aingizwa Mjini Marekani - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Sunday 19 November 2017

Malaika Aingizwa Mjini Marekani


Image result for Malaika Exavery music  pictures 
Msanii wa Bongo Fleva, Malaika Exavery.

MWANADADA anayefanya vizuri katika Bongo Fleva, Malaika Exavery ameeleza jinsi alivyotoswa huko Marekani, baada ya kuahidiwa kusimamiwa kazi zake, lakini asubuhi yake alipowafuata wahusika ili kuweka mambo sawa, wakamtosa.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Malaika alisema akiwa katika pub moja huko Los Angeles na marafiki zake wa Kitanzania, walimkutanisha na uongozi wa Justine Beiber kwa lengo la kusimamia kazi zake, wakakubali lakini kulipokucha jamaa hao walimweleza kwamba walimpa ahadi hiyo kwa sababu walikuwa mitungi na hawakuwa ‘siriaz’.

“Usiku jamaa walinihakikishia watasimamia kazi zangu, asubuhi na mapema nilikwenda kukutana nao ofisini kwao lakini waliniomba radhi kwa kile walichodai walinipa ahadi ile wakiwa ‘tungi’ hivyo natakiwa kusubiri hadi kumalizika kwa tour za Justine Beiber ili waangalie kama wanaweza kunisaini katika lebo hiyo,” alisema MalaikaImage result for Malaika Exavery music  pictures

No comments:

Post a Comment