Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora, kulingana na maafisa wa Japan na Korea kusini.
Kombora hilo limeonekana likianguka katika bahari ya Japan kulingana na chombo cha habari cha kitaifa cha Japan.Mapema mwezi Julai, Pyongyang ilidai kufanikiwa kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza.
Kombora hilo ni la hivi karibuni katika msururu wa makombora yaliofanyiwa majaribio hatua inayokiuka marufuku ya UN.
Umbali wa kombora hilo haujulikani.
Umbali wake umepingwa lakini wataalam wanasema kuwa linaweza kufika Alaska nchini Marekani.
Msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema kuwa kombora hilo lilirushwa na kwamba habari zaidi zinasubiriwa.
Kombora hilo la hivi karibuni ni la 14 kurushwa na Korea Kaskazini 2017.
Kombora hilo lilirushwa kutoka mkoa wa Jagang kaskazini mwa taifa hilo , kulingana na chombo cha habari cha Korea kusini Yonhap.
Katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan Yoshihide Suga alisema kuwa kombora hilo lilisafiri kwa takriban dakika 45 ikilinganishwa na kombora la masafa marefu lililofanyiwa majaribio mapema mwezi Julai.
Anasema kuwa lilianguka katika bahari ya Japan, lakini sio katika maji ya himaya ya Japan.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameitisha mkutano wa kiusalama katikati ya usiku kulingana na Yonhap
No comments:
Post a Comment