Rais John Magufuli
ameagiza kusimamishwa kazi kwa naibu kamishna wa uhamiaji kwa tuhuma za
kuingiza nchini humo raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi.
Kupitia
waziri mkuu Kassim Majaliwa kiongozi huyo ametaka kusimamishwa kazi
mara moja kwa bi Grace Hokororo na kuundwa kwa tume itakayochunguza
utoaji wa vibali vya uraia nchini humo.Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji kilichofanyika katika makao makuu ya uhamiaji jijini Dar es salaam.
Tayari Majaliwa amemuagiza waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kubuni tume hiyo ya uchunguzi.
Amesema kuwa haiwezekani raia wa kigeni kuingizwa nchini humo na baadaye kupewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina
source:bbc
No comments:
Post a Comment