Siku moja baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kupokea barua kutoka kwa
Mwenyekiti wa CUF Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili, Prof.
Ibrahim Lipumba inayoeleza kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti
Maalum na Madiwani wawili, Bunge limeridhia.
Leo July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika
Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi
zao ziko wazi.
Prof. Lipumba alitangaza kuwafuta uanachama Wabunge wanane na
Madiwani wawili kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kinidhamu, kukihujumu
chama, Kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge
hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo
hawana sifa za kuendelea na Ubunge.
Hivyo kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja
na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 kama ilivyojadidiwa
Mwaka 2015, Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na kumuandikia
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aendelee na hatua zinazostahili
kujaza nafasi hizo kwa mujibu wa Sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment