Katika video ya urefu wa zaidi ya dakika mbili, wavulana watano wa umri wa kati ya miaka 14 na 16 wanasikika wakicheka huku wakimrekodi kwa simu mtu mmoja aliyekuwa anazama kwenye bwawa jirani na nyumbani kwao Florida.
Licha ya mtu huyo kuomba msaada, wavulana hao waliendelea kulirekodi tukio hilo kwa simu huku wakicheka hatua za mwisho wa mhanga huyo wakisikika wakisema “Anakufa” lakini hawakwenda kutoa msaada wala hawakutoa taarifa.
Polisi wanasema tukio hilo lilitokea July 9, lakini wavulana hao licha ya kulirekodi hawakutoa taarifa kwa mamlaka hivyo kuufanya mwili wa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Jamel Dunn aliyekuwa na umri wa miaka 31 kukaa kwenye maji kwa zaidi ya siku nne hadi pale familia yake ilipotoa taarifa za kupotea kwake July 12 na mwili wake ukaopolewa kwenye maji July 14.
Wavulana hao hawatashtakiwa kwa sababu
Jimbo la Florida kwa sasa halina sheria zinazomlazimisha raia kutoa au
kutotoa msaada kwa yeyote:>>>”Kama ingalikuwepo (sheria ya namna hiyo) tungaliwashtaki.” Msemaji wa Idara ya Polisi ya Cocoa, Yvonne Martinez aliiambia CNN kwa njia ya simu
source:CNN
source:CNN
No comments:
Post a Comment