Duka La Jux Lakumbwa na Bomoa Bomoa - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 29 August 2017

Duka La Jux Lakumbwa na Bomoa Bomoa

Duka La Jux Lakumbwa na Bomoa Bomoa Mwenyewe Afunguka Haya

Duka La Jux Lakumbwa na Bomoa Bomoa Mwenyewe Afunguka Haya
Msanii Jux ambaye ni mmiliki wa duka linalo uza nguo za 'brand' yake ya 'African Boy', ametoa sababu iliyofanywa duka hilo lipitiwe na bomoa bomoa, katika eneo la Sinza jijini Dar es salaam.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Jux amesema duka hilo limevunjwa kwa sababu mwenye nyumba alikuwa na mgogoro na Mahakama kuhusu kiwanja hicho ndipo Mahakama ilipoamuru nyumba hiyo ivunjwe japo hawakupewa taarifa ya aina yoyote na mwenye nyumba huyo.

Nimepata hasara kubwa kwa kuvunjwa kwa jengo hilo kwa kuwa kuna baadhi ya vitu vimepotea pamoja na pesa taslimu shilingi Milioni moja imeibiwa na mpaka sasa, baba mwenye nyumba wangu hapatikani na sijui yupo wapi ?", alisema

No comments:

Post a Comment