WAKATI mashabiki wakiwa bado wanamshangaa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Massawe‘Wolper’ juu ya tabia yake ya kubadili wanaume kila kukicha, katika hali ya kushangaza, ameibuka na kudai kuwa ataendelea kubadili wapenzi, muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye, hana vigezo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alisema hawezi kuogopa maneno ya watu wanayosema juu yake kwa vile hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, kwani hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida. “Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Wolper.
Staa huyo aliongeza kuwa hata mtu aliyenaye hivi sasa endapo atagundua kama tabia haziendani, ataangalia ustaarabu mwingine kwani haogopi kusemwa kuhusu kubadilisha wapenzi.
Source : Risasi Mchanyiko
No comments:
Post a Comment