Kocha wa yanga George Lwandamina Apata msiba - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Wednesday 30 August 2017

Kocha wa yanga George Lwandamina Apata msiba

   Image result for picha za george lwandamina
                  KOCHA Mkuu wa Yanga George Lwandamina,

KOCHA Mkuu wa Yanga , Mzambia, George Lwandamina, amekumbwa na msiba mzito baada ya baba yake mzazi kufariki.
Lwandamina ambaye amejiunga na Yanga Novemba, mwaka jana, amempoteza baba yake huyo aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza ambapo amefariki usiku wa Jumanne August 29, 2017.
Lwandamina amesema: “Kutokana na msiba huo, natarajia kuondoka leo August 31 kwenda nyumbani Zambia kwa ajili ya mazishi na nikifika ndio tutajua tunazika lini kwani nasubiriwa mimi tu nifike.
“Baba alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kupooza na amefariki Jumanne usiku, nikienda huko nitakaa mpaka kila kitu kimalizike na natarajia kurudi Jumamosi ya wiki ijayo.”
olgertz inaungana na wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kumtakia pole George Lwandamina na familia yake kwa kuondokewa na mpendwa wao.

No comments:

Post a Comment