Waziri mkuu wa Tanzania mh kassim majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii
kutafuta mbinu bora za kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo
nchini ili kukuza sekta hiyo.
Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika mji wa kitalii wa Varadero ulioko kwenye mkoa wa Matanzas nchini Cuba.
Alisema mji wa Varadero tu unaingiza watalii zaidi ya milioni moja kwa
mwaka na unategemea kivutio kikubwa kimoja tu cha fukwe ambayo ina urefu
wa kilomita 22.
Aidha alisema idadi hiyo ni tofauti na Tanzania ambayo imejaliwa kuwa na
vivutio vingi vya utalii huku watalii wanaovitembelea ni wachache.
“Tunatakiwa kujitangaza zaidi.” alisema Majaliwa.
Waziri Mkuu alitaja baadhi ya vivutio vya utalii ambavyo ni mlima
Kilimanjaro, mbuga za wanyama, miji ya kihistoria ya Kilwa, Bagamoyo,
Stone Town pamoja na Mikindani.
“Vivutio vingine ni eneo la Oldvai George ambako binadamu wa kwanza
aliwahi kuishi, hifadhi ya Gombe ambako kuna sokwe ambao wanaishi kama
binadamu.”
Hata hivyo alisema Serikali itahakikisha jitihada zinafanyika katika
kukuza sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vilivyoko
nchini ili kuweza kuongeza idadi ya watalii.
Pia Waziri Mkuu aliwahamasisha Watanzania kujenga tabia ya kutembelea
vivutio vyeo vya utalii na kujifunza mambo mbalimbali na si kuwaachia
wageni pekee.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Sekta ya Utalii katika mkoa wa Matanzas,
Bw. Luis Martinez de Armas alisema mji wa Varadero ni kivutio kikubwa
cha utalii nchini Cuba.
Hata hivyo Bw. Luis alisema Tanzania inavivutio vingi vya utalii na
kwamba anavutiwa na mlima Kilimanjaro pamoja na wanyama na viumbe
vingine vilivyoko katika mbuga mbalimbali. Alisema wako tayari
kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya utali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment