Mh. Temba Anena haya Yamoto Band ilisambaratishwa na vigogo wenye Fedha - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Wednesday 27 September 2017

Mh. Temba Anena haya Yamoto Band ilisambaratishwa na vigogo wenye Fedha

Image result for Mh. Temba picture
Msanii wa Bongo Mh. Temba amedai kuwa chanzo cha kundi la Yamoto Banda kusambaratika ni baada ya watu wenye fedha kuingia kati.

Temba ambaye alikuwa msamamizi na mmoja ya waanzilishi wa kundi hilo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa imekuwa kawaida watu kuona vipaji viking’aa ndipo wanajitokeza kwa mgongo wa kusaidia lakini hawataki kuibua vyao na ndicho kilitokea kwa Yamoto Band.Image result for Yamoto Band

“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.

“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.

Kundi la Yamoto Band ambalo liliundwa na Aslay, Beka Flavour, Marombosso na Enock Bella kwa sasa kila mmoja anafanya kazi na menejiment yake.

No comments:

Post a Comment