
shamsa Ford na mumewe wake siku ya ndoa yao
UKITAKA kujua kichaa cha ‘Queen’ wa Bongo Muvi, Shamsa Ford, basi jaribu
kuichokonoa ndoa yake, na hicho ndicho anachokifanya mtu mmoja
aliyemfahamu kwa jina la Ilala Mjinga, ambaye kazi yake ni moja tu,
kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuhusiana na ndoa yake na mumewe,
Chid Mapenzi.
Kwa mujibu wa Shamsa ambaye siku chache nyuma alisema kuwa anamuona
jini-mkatakamba anainyapianyapia ndoa yake, hatimaye mambo yakamfika
shingoni na kuamua kushusha waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram,
akiwataka wale wote ambao wanadhani atakuja kuachana na mumewe, basi
wajue kwamba hiyo ni ndoto sawa na kusubiri embe dodo kwenye mti wa
korosho!
No comments:
Post a Comment