Mwanamuziki na aliyewahi kuwa mpenzi wa muigizaji Irene Uwoya, Msami
Baby amempongeza msanii mwenzake Dogo Janja kwa kufunga ndoa na
muigizaji huyo huku akiwasifu kwamba wameweza kuwabadilisha watu
kuhusiana na umri.
Msamii ametoa pongezi hizo leo kwenda kwa wawili hao baada ya Dogo Janja
kukiri kwa kinywa chake kwamba tukio linaloonekana kwenye picha
mbalimbali siyo kiki kama watu wanavyodhani bali ni ndoa kweli.
Msamii ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba "Ndoa ni jambo
la kheri sana, pongezi kwako Dogo Janja na Irene Uwoya mmefanya watu
wajue umri ni 'number' tu ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi" aliandika
Msami
Msami aliwahi kuwa kwenye mahusiano na muigizaji Irene Uwoya ambapo
karibuni alipokuwa kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa kila Ijumaa
alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na Uwoya alidai walishaachana na kudai
kwamba Uwoya ndiye aliyemtongoza mpaka kufikia kuwa wapenzi.
Friday 3 November 2017
Aliyekua mpenzi zamani wa Irene Uwoya amtumia Salamu za Pongezi Dogo Janja
Tags
# entertainment
Share This
About Unknown
entertainment
Labels:
entertainment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment