Harmorapa Aanza Mikakati ya kumnyapia Wema Sepetu - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Saturday 4 November 2017

Harmorapa Aanza Mikakati ya kumnyapia Wema Sepetu

Image result for Harmorapa pictureMsanii wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa ambaye hakauki kwenye mitandao kwa vitendo vyake vya kiki, amesema na amini naye ipo siku atatimiza ndoto zake na kumuoa Wema Sepetu kama alivyofanya Dogo Janja kwa Uwoya.

Kwenye ukurasa wake wa instagram, Harmorapa ameandika ujumbe akisema kwamba hatokuja kukata tamaa juu ya ndoto yake ya kumng'oa 'Tz Sweetheart'Wema Sepetu na hatimaye kumuweka ndani kama mke wake.


“Naamini sana katika ndoto kua ipo siku ndoto unayoota itatimia na kuwa kweli, sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja, naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake, nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakua wangu, ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini, kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia... One day you will be mine Wema Sepetu”, ameandika Harmorapa.Image result for Harmorapa picture

No comments:

Post a Comment