Korea Kaskazini imesema kuwa
imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM,
wakitaja kuwa onyo kali kwa Marekani.
Kiongozi wa Korea Kaskazini
Kim Jong-un alisema kuwa jaribio hilo lilibaini kwamba marekani yote ipo
katik radara ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa, vyombo vya
habari vimeripoti.Jaribio la kombora hilo linajiri wiki tatu baada ya jaribio la kombora la kwanza la masafa marefu la Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani Donald Trump amelitaja jaribio hilo kuwa la kijinga na kitendo cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini .
China pia imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pandfe husika zilizo na waiwasi kujizuia ili kutoendeleza wasiwasi zaidi.
Ikithibtisha kurushwa kwa kombora hilo, Korea Ksakzini ilisema kuwa kombora hilo la masafa marefu liliruika kwa dakika 47 na kufika urefu wa kilomita 3,724.
Imesema kuwa jaribio hilo lilifanikiwa kujaribu uwezo wa kombora hilo kuingia.
Kiongozi huyo pia alisema kuwa jaribio hilo lilithibitisha kwamba Korea Kaskazini sasa ina uwezo wa kushambulia ardhi yoyote ya Marekani kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
source:bbc dira ya dunia
No comments:
Post a Comment