Afisa mmoja wa kampuni ya uchimbaji
madini kutoka Canada Acacia alizuiliwa kwa muda nchini Tanzania alipouwa
akijaribu kulitoroka taifa hilo , kampuni hiyo iemsema katika taarifa.
Taarifa
hiyo imesema kuwa afisa huyo mwandamizi alizuiliwa kwa muda huku cheti
chake cha pasipoti kikihukuliwa katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere.Kisa hicho kinafuatia shinikizo za serikali kwa wafanyikazi wa kampuni hiyo katika kipindi cha saa 48 zilizopita, taarifa ilisema.
Mapema wiki hii Acacia ilisema katika taarifa kwamba serikali iliiambia kwamba inafaa kuilipa Tanzania dola bilioni 190 kupitia kodi, adhabu na riba.
Kampuni hiyo imekana na imechapisha habari hizo katika mtandao wake ili kupinga madai hayo
source bbc dira ya dunia
No comments:
Post a Comment