Naitwa Beatrice francic chekibula mwenyeji wa TaNGA ila
asaivi naishi dare s salaam nasumbuliwa na vidonda sehemu za siri vilianza kama
kipele kimoja kikambatana na muwasho nkawa najikuna vikaja kuwa vingi na kunipa
maumivu makali hata usiku sipati usingizi kutokana na maumivu nayopitia hivi sasa ni
mwaka wa3 tangia ili tatizo linianze.
Nateseka sana hospital ni nyingi nimeshazunguka sana nkaenda mpaka OCEAN ROAD wamenambia niende nkukata nyama nilishindwa
kutokana hali yangu ngumu kwani nliambiwa nipeleke 80000 ili nifnyiwe vipimo
kutokana na uwezo sina sijaweza kurudi tena Ocean road ,vidonda vipo chini
kabisa kiasi ambacho ata kupata haja nishida tabu mateso kutokana na maumivu
nayopata.
Aliyekua mume wangu kanikimbia kwasababu ya shida yangu nkimpigia simu
anipokelei na sanyingine ananiuliza
nimsahau nini? Au una ahadi gani na
mimi?tuloahidiana anisaidii kwa lolote lile na kapata mwanamke mwingine ambae
wapo wote wanaishi pamoja.na nimejaliwa kupata
watoto 2 wakwanza wakike wapili wakiume lakini msaada wangu huyu mdogo
ambae wakiume.
Maumivu haya yananifanya na meza DICLOPA 4 kwa mpigo ili
nipunguze maumivu lakini havisaidii
chochote kutokana na haya maumivu naweza
nkakaa siku3 sili hapa unavoona nakaliya mgongo na si makalio sababu siwezi
kukaa kitako kwa jinsi navosikia maumivu .kama hapa kodi yanyumba i nadaiwa
ndugu zangu nao nikiwaomba msaada wananiambia hali ngumu hiyo pesa awana ndonajikuta na baki na mateso
yangu.
Kwani apo zamani mimi ndolikua mtafutaji kwa wanangu nilikua
nafanyakazi kwenye company ya bora,ataivo nilivopata shida iyapa sikuwai kwenda
kutoa taarifa kiwandani bora kwani nauli ilikua kikwazo unajikuta hiyo hela
ya nauli ni vema upike chakula ule na watoto.
Nawaomba watanzania wanisaidie kwani sina uwezo wakwenda hosptali
kujitibia tu shida kwani mwanangu mdogo
ndie tegemeo langu natamani na mim
nipone nirudi kwenye hali yangu ya zamani ili nisaidiane na mwanangu huyu mdogo
si mdogo kiivo ivi sasa ana umri 18 ndo hakikishe nipate ugali nawaombeni sa
ndugu zangu mnisaidie kwani sina msaada
wowote ule sibagui mimi mwenye chochote napokea kwani nateseka sana.
No comments:
Post a Comment