MIEZI michache ikiwa imepita tangu mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza nyago, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ahongwe gari aina ya Benzi, amekumbwa na aibu ya mwaka kufuatia kuporwa na aliyekuwa mpenzi wake baada ya kusikia tetesi kuwa na uhusiano wa karibu na mwanamuziki, Hamad Ally ‘Madee’.
Kwa mujibu wa chanzo, mwanamuziki huyo alikuwa akitokea kwenye mgahawa uitwayo Rapsody, ambapo alipofika maeneo ya Salenda gari lingine lilipita mbele yake na kumziba ambapo mpenzi wake huyo alishuka ndani ya gari na kumuomba ampe funguo.
“Unajua mambo mengine ni wivu tu wa kimapenzi ni kweli alinifanyia hivyo kwa ajili ya Madee, wakati huyo ni kama kaka yangu lakini nashukuru Mungu baada ya hali kutulia amenirudishia gari,” alisema Lulu.“Yaani ilikuwa ni aibu kwa Lulu, kwanza mavazi aliyovaa hayaelezeki hata kidogo na mpenzi wake huyo aliomba washuke wote kwenye gari huku akimwambia kuwa aendelee na Madee hivyo amuachie gari lake,” kilisema chanzo.
Star Mix lilimtafuta Lulu ili kuthibitisha madai hayo, ambapo alikiri kufikwa na masaibu hayo
No comments:
Post a Comment