Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini uliimarika - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Saturday, 22 July 2017

Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini uliimarika


Uchumi wa Korea Kaskazini
Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini uliimarika kwa haraka katika kipindi cha miaka 17 iliopita licha ya kuwekewa vikwazo kutokana na mpango wake wa kinyuklia na utengenezaji wa makombora ya masafa marefu.
Uzalishaji wa bidhaa nchini humo ulikuwa kwa asilimia 3.9 2016 ikilinganishwa na mwaka uliopita kulingana na benki ya Korea.
Ukuwaji huo unatokana na uchimbaji madini, kawi na uuzaji wa bidhaa nchini China.
Marekani imekuwa ikiitaka Beijing kukata biashara na Pyongyang huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu mipango ya kinyuklia ya rais Kim Jong Un.
China ndio mshirika pekee mkuu wa Korea Kaskazini na mfadhili mkubwa wa misada nchini humo.
Wiki iliopita China ilitoa data ikidai kuwa Korea Kaskazini haina uwezo mkubwa kama inavyodaiwa na rais Trump.
Lakini huku Beijing ikisitisha ununuzi wa mkaa kutoka Korea Kaskazini, imeendelea kufanya biashara ya chuma na bidhaa nyengine.
Ijapokuwa Korea Kaskazini haichapishi data za kiuchumi , benki kuu ya Korea Kusini inatoa takwimu za ukuwaji kila mwaka kutokana na data yake kutoka katika wizara ya muungano na hudumu za kijasusi.
Ukuwaji mkubwa wa Korea Kaskazini 2016 ndio mkubwa zaidi tangu ukuwaji ule uliorekodiwa 1999.
Na ukuwaji wa mwaka uliopita unatokana na ule wa 2015 baada ya uchumi wa Korea Kaskazini kunyauka kwa asilimia 1.1 kufutia mporomoko wa bei za bidhaa duniani ambao uliathiri thamani ya mkaa wake na chuma.
Raia wa Korea kaskazini ni miongoni mwa watu masikini duniani huku pato la kitaifa likiwa dola 1136 kwa mwaka.
Uchumi wa Korea Kusini ni mara 20 ya mapato hayo.
Wasiwasi wa kimataifa kuhusu Korea Kaskazini uliongezeka wiki iliopita baada ya jaribio la kombora la masafa marefu , ambalo inaamini lina uwezo wa kufika Alaska nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment