Aliyekuwa video vixen mkali kutoka Bongo Agnes Masogange amefunguka kuhusu maisha yake huku akigusia kuwa watanzania wengi wanapenda kumponda bure.
Katika mahojiano yake na Gazeti la Mwanaspoti mrembo huyu alisema Kuwa hana dhiki ikiwa atafikia kiwango cha kuuza mwili wake ili ajitafutie. Masogange alisema,
“Watu bana!, mimi sina dhiki ya kufikia kuuza mwili wangu eti nipate pesa na kuhusu zile picha kipindi kile nilizopiga hazikuwa za utupu sema basi tu watanzania tunapenda kuzusha sana. Na mtu kuenda Sauzi ndio ameenda kujiuza?,” Masogange aliliambia Gazeti la Mwanaspoti.
Aliongeza kuwa hakuna mtu anayemnunulia mavazi anayovaa wala kumpa pesa ya matumizi yake kwa hivyo hakuna anayeweza kumwambia chochote.
“Mimi nilikuwa na biashara zangu nafanya na wanaosema hivyo hawanisaidii chochote,hakuna mtanzania anayeninunulia nguo,hayupo anayenipa pesa waongee tu. Unajua sisi wadada tuna tabia ya kuoneana wivu akiona unafanya vizuri anaanza kukusemea vitu vya ajabu pembeni

No comments:
Post a Comment