Chidi Benz azua jipya mjini, adai 2Pac yuko hai na anaishi nchini Cuba, na wanaongea kila siku na tayari ameshafanya naye ngoma itakayotoka hivi karibuni.
Chidi Benz ambaye kwa sasa anazungumzwa sana kwa skendo za utumiaji wa madawa ya kulevya, akiongea na eNewz alisema kuwa "Maneno yanayoongelewa kwamba 2Pac amefariki siyo kweli, Kila siku ninaongea na 2pac na hata sasa hivi nimetoka kuongea naye"
Mimi na 2Pac tumekutana Cuba, na tumefanya nyimbo ya pamoja na Mungu akisaidia hivi karibuni tataachia nyimbo hiyo".
"2Pac ana mpango wa kurudi kwenye muziki, na wimbo wetu tuliorekodi ndiyo utamrudisha. Na hivi karibuni 2Pac atakuja bongo, ila atakuja kimya kimya kama alivyokuja Beckam" Aliongeza Chidi Benz.
Pia Chid aliendelea kwa kusema "Baada ya kukutana na 2Pac tuliamua kurekodi baadhi ya vipande vya video ambavyo tutaanza kuvisambaza kwanza ili kuweza kuwajulisha watu kuwa 2Pac bado yupo hai na kuwaondoa watu fikra za kuwa 2Pac ni marehemu".
Hata hivyo kitu cha kushangaza zaidi ni baada ya Chid kuendelea kusema kwamba anamdai 2Pac kipini chake cha puuani ambacho alimuazima walipokuwa wote nchini Cuba.
Kama ilivyokuwa kwa Young Dee, Chid Benz naye ameonekana kuwa na hali ya kujichanganya sana katika maelezo yake kila aanapoongea.
""Hivi karibuni Ali Kiba akiongea na eNewz alishauri serikali iingilie kati suala la Chid Benz na kumpatia matibabu. Na hata kama akibainika anajihusisha na madawa Alikiba alishauri "Chid asifungwe bali apelekwe 'rehab' akatibiwe kwani kumfunga mtu anayetumia madawa ni kumtesa tu
No comments:
Post a Comment