Msanii wa muziki na video vixen, Amber Lulu Jumanne hii alipelekwa kituo
cha polisi cha Urafiki Ubungo jijini Dar es salaam kueleza kama
anahusika katika kusambaza picha chafu mtandaoni ambazo zinamuonyesha
akiwa nusu uchi na rapa Young Dee.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata, zinadai kwa sasa muimbaji huyo
yupo nje baada ya kuhojiwa kwa masaa machache kuhusiana na tukio hilo.
Akiongea na Bongo5 Jumaatano hii shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka
jina lake litajwe, amesema mrembo huyo alishikiliwa na kituo hicho kwa
masaa matatu na baada ya hapo aliachiwa.
“Ni kweli Amber Lulu alikuja na tulimuona hapa kituoni jana kama jioni
jioni hivi,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka atajwe jina lake.
Shuhuda huyo alidai mrembo huyo alifika kituoni hapo akiwa na team yake
ya uongozi kutoka Afrika Kusini pamoja na uongozi wa Young Dee.
Bongo5 ilimtafuta meneja wa Young Dee ili kuzungumzia sakata hilo lakini
meneja huyo hakuwa anapokea simu hata hivyo alivyotumiwa meseji alisema
bado wanalishughulikia tatizo hilo na pale watakapokuwa na taarifa
rasmi wataitoa kwa jamii
Wednesday, 30 August 2017
Home
habari za wasanii
picha: Amber lulu akifika kituo cha polisi baada issue nzima ya picha za utupu
picha: Amber lulu akifika kituo cha polisi baada issue nzima ya picha za utupu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment