Mbunge wa Viti Maalumu (CUF) aliyevuliwa ubunge hivi karibuni Salma
Mwasa amesikitishwa na kitendo cha askari wa Manispaa ya Ubungo cha
kutaka kumzuia asikanyage kwenye halmashauri hiyo.
Mwasa ni miongoni mwa wabunge kumi waliovuliwa uanachama sanjari na
madiwani wawili wa CUF kwa madai ya kukihujumu chama hicho, hali
iliyosababisha kukosa fursa za kuwa wabunge.
Akisimulia tukio hilo lililotokea leo Jumatatu, Julai 31, Mwasa amesema
aliitwa na askari hao na kuambiwa hatakiwi kuonekana katika eneo hilo la
manispaa na kwamba, hiyo ni amri kutoka juu kwa wakubwa.
“Mimi ninachojua amri zipo kumi tu, sasa hiyo 11 inatoka wapi? Lakini
niliwaeleza kwamba mimi ni mkazi wa Ubungo sasa mnaponizuia nisije hapa
hamnitendei haki kwa sababu nakuja kufanya mahitaji mbalimbali,”
amesema.
“Mimi nimekuja kama mwananchi wa kawaida. Naomba umma utambue mimi bado
ni mbunge hapa nilipo nina barua ya uteuzi na sina barua ya utenguzi,”
anasema Mwasa.
Hata hivyo, haikuwa rahisi askari hao wa manispaa kumtambua Mwasa badala
yake walikuwa na karatasi yenye majina mawili yaliyoandikiwa Salma
Mwasa na diwani wa viti maalumu Leila Hussein, ambao hakutakiwa
kuonekana eneo hilo wakati kikao cha Baraza Madiwani kikiendelea.
Askari hao walitumia njia za kuwauliza watu mbalimbali wakiwamo
waandishi kama wanawafahamu kina Mwasa na Leila na walipowauliza
wanashida nao gani walijibu hawatakiwi kuingia ndani ya ukumbi wa
mikutano
Tuesday, 1 August 2017
Home
Unlabelled
hapotoshi CUF mbunge alovuliwa ubunge azuiliwa kuingia katika kikao cha madiwani
hapotoshi CUF mbunge alovuliwa ubunge azuiliwa kuingia katika kikao cha madiwani
Share This
About Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment