Hii leo Manchester United wamekamilisha usajili wao wa tatu
baada ya kumnunua kiungo Nemanja Matic kutoka Chelsea usajili ambao
umekuwa ukitajwa kwa muda mrefu sana.
Mourinho amekuwa akimhitaji Matic kwa muda sasa na kiasi cha £39.7m
kimetosha kumsaini Matic na kumpa mkataba wa miaka mitatu huku kukiwa na
kipengele cha kuongeza mwaka mmoja hapo baadaye.
Usajili wa Matic aliyepewa jezi namba 31 una faida kubwa kwa Paul
Pogba ambaye amekuwa na msimu usio mzuri sana toka ajiunge na Manchester
United tofauti na wakati akikipiga Juventus.
Pogba bado ni bora lakini kuna vitu anakosa United ambavyo alikuwa
akivipata alipokuwa Juventus na hii ndio imempa mzigo mkubwa sana ndani
ya United kiasi cha kupelekea makali yake kutoonekana.
Wakati
akiwa Juventus Pogba alikuwa akicheza mbele ya viungo watatu Andrea
Pirlo,Marchisio na Sami Khedira lakini akiwa United alirudi nyuma na
wakati mwingine alicheza mbele ya mabeki na hii ikamfanya kupotea.
Matic anakuja United na Mourinho anaweza kujaribu kuchezesha 4-3-3 au
4-2-31 na mifumo yote hii inamfanya Pogba kuwa mbele ya viungo wawili
ambao wanaweza kuwa Hererra na Matic,Fellaini na Matic au Carrick na
Matic.
Matic wakati akiwa Chelsea uimara wake na ukabaji wake vilimfanya
Cesc Fabregas ambaye alianza kuonekana kupotea kama ilivyo kwa Pogba
lakini kiwango cha Matic kilimfanya Fabregas kupiga assists 18 msimu wa
2014/2015 na Chelsea wakabeba ndoo.
Lakini ujio wa Matic unaweza kuwa habari mbaya kwa Marouane Fellaini
ambaye tayari kocha wake Jose Mourinho ameshasema ni rahisi kwake
kuondoka kuliko kumuuza Fellaini kwenda klabu yoyote.
Msimu uliopita Fellaini amesota sana benchi na kiwango cha Ander
Herrera kilimfanya kuzima kabisaa na mara nyingi akatumika kama mchezaji
wa ziada akiingia kipindi cha pili cha mchezo.
Ujio
wa Matic unaweza kumfanya Fellaini kupotea kabisa kwani Matic kuna
uwezekano mkubwa akapewa muda mwingi wa kucheza na pia Herrera huwezi
muweka nje, ni wazi kwamba Fellaini atazidi kukaa nje.
Huu ni usajili wa 3 wa United msimu huu baada ya Victor Lindelof na
Lukaku, nani atafuata kusajiliwa baada ya Nemanja Matic?ni Ivan Perisic
kutoka Inter Millan au United watakamilisha usajili wa Serge Aurier toka
PSG
source shaffih dauda.
Tuesday, 1 August 2017
Home
Unlabelled
Nemanja Matic amwaga wino United, ni kicheko kwa Pogba na kilio kwa Fellaini
Nemanja Matic amwaga wino United, ni kicheko kwa Pogba na kilio kwa Fellaini
Share This
About Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment