inasadikika Hedhi uwa jambo mwiko kuonekana mbele ya kadamnasi.
Msichana wa umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi
kusini mwa India amejiua baada ya mwalimu wake kumuaibisha kwa sababu ya
hedhi.Katika ujumbe alioacha wakati wa kujiua, alidai mwalimu wake "alimtesa".
Ingawa
msichana huyo hakutaja kisa hicho cha kuaibishwa kwa sababu ya hedhi,
mamake msichana huyo anasema aliagizwa na mwalimu wake kutoka nje ya
darasa baada kwa sababu ya doa la damu ya hedhi lililokuwa kwenye nguo
zake.
Hedhi ni mwiko kuzungumziwa hadharani India.
Wanawake kitamaduni huaminika kuwa wachafu au hata waliolaaniwa wakati wanapopata hedhi.
Polisi wanasema wamepata ripoti za kisa hicho cha kujiua na wanafanya uchunguzi.
Kisa hicho kilitokea Jumapili katika wilaya ya Tirunelveli siku ya Jumapili katika jimbo la Tamil Nadu.
"
Sijui
ni kwa nini mwalimu wangu analalamika kunihusu. Bado sielewi ni kwa
nini ananihangaisha na kunitesa hivi," mwanafunzi huo aliandika kwenye
barua yake
Alianza barua hiyo: "Amma (mama), tafadhali nisamehe."
Mamake mwanafunzi huyo anadai mwalimu huyo alimchapa binti yake siku za awali kwa kutofanya kazi yake ya ziada.
"Binti yangu alipata hedhi akiwa shuleni Jumamosi iliyopita," mamake ameambia BBC Tamil.
"Alipomjulisha mwalimu wake, alipewa kitambaa cha kupangusa ubao atumie kama sodo.
"Mwalimu alimfanya binti yangu kusimama nje ya darasa. Msichana wa miaka 12 atavumiliaje aibu ya aina hiyo?" alishangaa.
Msichana huyo alijiua siku moja baadaye.
Thursday, 31 August 2017
Mapya haya: Binti wa miaka 12 Ajiuwa kisa Hedhi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment