Chelsea wamsajili Drinkwater kutoka Leicester - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Thursday, 31 August 2017

Chelsea wamsajili Drinkwater kutoka Leicester


Danny Drinkwater  Danny Drinkwater alicheza mechi 35 na kuwasaidia Leicester kushinda Ligi ya Premia 2015-16
Chelsea wamemnunua kiuungo wa kati Danny Drinkwater kutoka Leicester City kwa £35m.
Mchezaji huyo wa miaka 27 alichangia sana katika kikosi cha Leicester kilichoshinda Ligi ya Premia msimu wa 2015-16 lakini aliomba kuihama klabu hiyo baada ya kutambua kwamba atafutwa na Chelsea.
Chelsea pia wamemnunua beki Davide Zappacosta kutoka Torino kwa mkataba wa miaka minne kwa ada ambayo haijafichuliwa.
Hata hivyo, mshambuliaji Fernando Llorente ameamua kwenda Tottenham badala ya Stamford Bridge.
Na kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley alibadilisha nia yake kuhusu kuhamia katika klabu hiyo ya Antonio Conte.
Leicester wanatarajia kumsajili Adrien Silva, 28, kutoka Sporting siku ya Ijumaa kwa £22m kujaza nafasi ya Drinkwater.

No comments:

Post a Comment