Mke wa Roma: napata wivu kila napo sikia jina la Mange Kimambi - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Thursday 31 August 2017

Mke wa Roma: napata wivu kila napo sikia jina la Mange Kimambi

Image result for mke wa roma
                                           pichani Roma na mkewe siku ya harusi

Kwenye mitandao ya kijamii August 30, 2017 gumzo lilikuwa post ya mke wa Roma Mkatoliki, Mama Ivan kwenye Instagram yake baada ya kuelezea kipande cha wimbo mpya wa Roma ‘uku ama kule' akisema kila anapokisikia hupata wivu.

Licha ya kudai kuwandika maneno hayo kama utani huku wengi wakiyachukulia serious hadi kupelekea Mange Kimambi kuyanasa na kisha kuya post kwenye Istagram na kumuomba Mke wa Roma amruhusu awe mke mwenza ili amsaidie kumlinda Roma asiibiwe na wanawake wangine.

Mke aliandika Instagram...“Kiukweli kila nikisikiaga huu msatari napata sanaaa wivu, utani utani hivi hivi mwisho wa siku inakuwa kweli, mimi mwenyewe alinianza kiutani utani hivi hivi, yani nyie!! wanaume hawa!! Kuolewa na msanii kunahitaji moyo” – Mke wa Roma

Mke wa Roma alihojiwa na kufunguka akisema hakuwa serious bali kama Roma ataamua kumuowa Mange hatakuwa na usemi kwa kuwa mwanaume ndio mwenye maamuzi ingawa amedai hategemei kuona akioa mke mwingine kwa sababu dini hairihusu.

No comments:

Post a Comment