ni balaa...Rais wa TLS Tundu Lissu Ameitisha Mgomo - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Sunday 27 August 2017

ni balaa...Rais wa TLS Tundu Lissu Ameitisha Mgomo


                        Raisi wa mawakili tanzania akizungumza na wandishi wa habari mapema leo.


Mwanasheria mkuu wa CHADEMA na Rais wa chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Mhe Tundu Lissu, amewataka mawakili wote nchini kugoma kwenda mahakamani siku ya jumanne na jumatano, kuonesha kupinga vitendo walivyofanyiwa mawakili wenzao wa IMMMA, ambao ofisi yao imechomwa moto.


Tundu Lissu amesema kitendo hicho kinaingilia uhuru wa wanasheria na taaluma ya sheria pia kinahatarisha uhuru wa mahakama na utawala wa sheria kwa ujumla huku akiwataka mawakili wote nchini walio chini ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS),  kutokwenda  mahakamani kufanya kazi zao.

“Baraza la uongozi linawataka wanachama wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria katika mahakama pamoja na mabaraza ya aina zote kati ya siku za jumanne na jumatano ya tar 29 na 30 Agosti 2017, kwa lengo la kuwaunga mkono mawakili wa IMMMA, na kuonyesha kutokukubaliana kwetu na vitendo vya kihalifu vya kuwashambulia mawakili hao kwa mabomu”, amesema Mhe Tundu Lissu leo kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.

SOMA ZAIDI- Nimeshtushwa na tukio la bomu kwenye Ofisi ya Mawakili – Zitto

Hata hivyo Tundu Lissu amesema Ofisi za IMMMA Advocates zimelipuliwa kwa mabomu na kusababisha baadhi ya nyaraka kupotea kitu ambacho kitawafanya Mawakili hao kushindwa kufanya kazi kiufasihi.

“Mawakili wa IMMMA wameshambuliwa ofisi zao zimepigwa mabomu, nyaraka zimepotea zingine zimeungua moto, hawataweza kwenda mahakamani kwa sababu vitendea kazi vyao vimeharibiwa, sisi mawakili wengine wote nchi nzima, tuna wajibu wa kuwaunga mkono mawakili wa IMMMA kwa kutoenda mahakamani vile vile, akiumizwa mmoja tumeumizwa wote, kwa hiyo tunawataka wanachama wetu popote walipo kesho kutwa wasiende mahakamni, wasiende kwenye mabaraza yoyote ili kuwaunga mkono wenzetu ambao wameshambuliwa”,amesema Lissu.

Mpaka sasa ni siku moja tangu ofisi ya za mawakili wa IMMMA zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam kuungua moto  na waliohusika na uhalifu huo bado hawajajulikana

No comments:

Post a Comment