Polisi Rwanda wafanya msako nyumba ya aliyetaka kuwania urais - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Wednesday 30 August 2017

Polisi Rwanda wafanya msako nyumba ya aliyetaka kuwania urais


Diane Shima RwigaraPolisi nchini Rwanda wamekanusha kwamba wanamzuilia mwanamke aliyetaka kuwania urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu.
Taarifa zilikuwa zimeenea mitandao ya kijamii nchini humo kwamba polisi wamemkamata Diane Shima Rwigara na mamake.
Msemaji wa Polisi ya Rwanda Theos Badege ameiambia BBC kuwa polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake kama sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu makosa anayotuhumiwa yeye na familia yake ambayo ni pamoja na kosa la kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi.
Taarifa zilikuwa zimesema kuwa watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha lakini walivalia mavazi ya kiraia walivamia nyumbani kwa mwanasiasa huyo mapema leo Jumatano.
Familia yake inasema kufikia sasa bado mwanamke huyo na mamake hawajulikani waliko.
Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu ambapo Rais Paul Kagame alishinda kwa kura nyingi.
Mwanasiasa huyo, ambaye amekuwa akitetea haki za wanawake nchini humo, baadaye alianzisha kundi la kukosoa utawala wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment