mfano wa picha ya ukuta utakao jengwa
Utawala wa rais Donald Trump
umechagua makampuni manne kwa kazi ya kujenga sampuli ya ukuta ambao
rais Trump ulitangaza sana juu ya mpaka wa Mexico na nchi yake.
Ukuta
huo ulikuwa ni miongoni mwa vipaumbele vya kwanza vya rais Trump na
kuzusha sintofahamu na kusababisha maandamano pande zote mbili.Naibu Kamishna Ronaldo Vitiello,ambaye pia ni mkuu wa doria katika mpaka wa Marekani amewaambia waandishi habari kwamba mikataba ya ujenzi wamepatiwa makampuni kutoka Alabama Arizona, Texas na Mississippi.
Inaelezwa kuwa gharama halisi za ujenzi huo zinakadiriwa kuwa hadi dola milioni unusu. Wakati wa kampeni zake rais Trump amesisitiza kwamba Mexico watalipa gharama ya ukuta huo. Sampuli hiyo ya ukuta itajengwa mjini San Diego, California.
No comments:
Post a Comment