MWASHIUYA: NILIFUNGA BAO ALIKIBA AKANIPA TSH. 120,000/= - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Thursday, 31 August 2017

MWASHIUYA: NILIFUNGA BAO ALIKIBA AKANIPA TSH. 120,000/=


Geofrey Mwashiuya na Alikiba.

MCHEZAJI wa Klabu ya Yanga, Geofrey Mwashiuya amefunguka kuhusu alivyofunga bao kwenye moja za mechi aliyoitumikia klabu hiyo na kujikuta akizawadiwa pesa kiasi cha Tsh. 120,000/= na mwanamuziki mkali wa ngoma mpya ya Seduce Me, Alikiba.
Mwashiuya ambaye kwa sasa ni majeruhi na hajaingia uwanjani tangu msimu mpya wa 2017/2018 uanze, amefunguka hayo wakati akifanya mahojiano kwenye Kipindi cha SpotiHausi kinachorushwa LIVE kila Alhamisi saa 10:00 jioni kupitia Global TV Online.
Mkali huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Kimondo FC ya jijini Mbeya ameeleza namna ambavyo amekuwa akishirikiana na wachezaji wenzake wa Yanga huku akianaika mikakati yake ya kwenda nje ya nchi kupiga soka la kulipwa.
Licha ya kumtaja kwa jina mchezaji aliyekuwa akimkubali ndani ya Yanga, pia amezikana tetesi alizohusishwa nazo za kutaka kujiunga na Azam FC ama Singida United ambapo ameeleza kuwa yeye bado ni mchezaji halali wa Yanga na ana mkataba na klabu hiyo, hivyo hajawahi kufikiri kwenda Azam au Singida Utd.

No comments:

Post a Comment