Zamaradi Mketema aonyesha mapenzi yake kwa Aslay - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Monday, 28 August 2017

Zamaradi Mketema aonyesha mapenzi yake kwa Aslay

ZAMARADI MKETEMA: MUZIKI KWA SASA UPO KWA ASLAY TU

MUZIKI KWA SASA UPO KWA ASLAY
WASWAHILI wanasema mapenzi ni kikohozi na kuyaficha huwezi. Msemo huu umedhihirika kwa mtangazaji wa kituo cha televisheni, Zamaradi Mketema, ambaye ameweka wazi mapenzi aliyo nayo na anavyomkubali msanii, Aslay, kimuziki.
Zamaradi ameonyesha wazi kumkubali zaidi Aslay, anayetamba na ngoma zake kama Likizo, Baby, Pusha na nyingine nyingi, kuliko msanii yeyote yule, na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka mambo hadharani.
MUZIKI KWA SASA UPO KWA ASLAY TU
“Tukiacha utimu ambao hauna ubaya labda ndiyo unafanya kuwe na uhai wa muziki na kupatikane vitu vya kuongelea, ila muziki kwa sasa upo kwa Aslay.
“Natamani Watanzania wangemwelewa katika hali ya ukubwa aliyo nayo, najua wanamtambua ila natamani tu wangemtambua zaidi; huyu mtoto ni habari nyingine,” ameandika Zamaradi.

No comments:

Post a Comment