kocha wa Timu ya Arsenal, Arsene Wenge
Wenger, Wenger, Wenger hilo ndio jina linalotawala midomo ya mashabiki wa klabu ya Arsenal. Japokuwa wapo wachache wanamuamini Mfaransa huyo lakini wengi hawana imani na Mfaransa huyo.
Kipindi cha usajili suala la Alexis Sanchez lilitawala sana vichwa vya habari lakini habari njema ni kwamba Arsenal walifanikiwa kupambana na Alexis Sanchez amebaki katika timu yao.
Kocha Arsene Wenger amesema kubaki kwa Sanchez ilikuwa jambo muhimu sana kwao japokuwa dirisha la usajili halikuwa zuri sana kwao lakini ana imani kubwa Sanchez atakuwa katika kiwango kizuri na atawasaidia sana.
“Mapema sana atarudi katika kiwango chake kikubwa, dirisha la usajili limemalizika na Sanchez ni mchezaji wetu na atakuwa na malengo kuhusu klabu yetu” alisema Arsene Wenger.
Kuhusu kiwango cha timu Wenger amesema ni mechi tatu tu zimechezwa na matokeo yaliyotokea hana furaha nayo lakini safari bado ni ndefu na anaweza kupambana na kubeba ubingwa wa Epl.
“Bado michezo 35 inamaanisha safari bado ni ndefu sana na viwango vya wachezaji vinabadilika muda wowote tunaweza kuwa vizuri sana na chochote kitatokea” alimalizia Arsene Wenger.
No comments:
Post a Comment