Majaribio ya bomu la nyuklia ambayo
yalifanywa na Korea Kaskazini Jumapili yalisababisha maporomoko kadha
ya ardhi, kwa mujibu wa picha za satelaiti ambazo zinaaminika kuwa za
kwanza kabisa za eneo ambalo majaribio hayo yalifanyika.
Majaribio
hayo ya bomu yalifanyika chini ya ardhi katika eneo la kufanyia
majaribio silaha linalotumiwa na Korea Kaskazini la Punggye-ri ambalo
lina milima mingi.Kundi la uchunguzi kwa jina 38 North limechapisha picha ambazo zinaonekana kuonyesha "maporomoko kadha katika eneo kubwa" kuliko yaliyowahi kushuhudiwa awali.
Mlipuko wa bomu hilo ulisababisha tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 kwenye vipimo vya Richter.
No comments:
Post a Comment