Dk. Vincent Mashinji
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali tukio la Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa na watu wasiojulikana jana Alhamisi, mchana.
Akizungumza na wanahabari leo, Naibu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Safari amesema kuwa chama chao kinalaani tukio hilo kuwa ni la kinyama ambapo amesema serikali haitakiwi kulifumbia macho hata kidogo.
Amesema siku za hivi karibuni Lissu alitoa taarifa kwa wanahabari kuhsu gari linalomfatilia na kwamba watu hao ameshawabaini lakini jeshi la polisi halikuchukua hatua.
Aidha Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kuwa Tundu Lissu amezinduka leo asubuhi akiwa katika Hospitali ya Aga-Khan jijini Nairobi nchini Kenya, kwa sasa ameshazinduka anajitambua na anaendelea vizuri
No comments:
Post a Comment