Vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha picha za waandamanaji wakilala barabarani usiku
Vikosi vya usalama nchini Togo vimerusha gesi ya kutoa machozi mapema leo, kutawanya mamia ya waandamaji wanaoipinga seikali walioshinda usiku kucha mjini Lome.Polisi walichukua hatua ya maandamano ya nchi nzima ya saa 48 ya kutaka kumalizika kwa utawala wa miaka 50 wa familia ya Gnassingbe
Hakuna taaraifa yoyote ya majeruhi au maafa.
Maandamano yaliendelea licha ya Rais Faure Gnassingbe, kuahidi kurejesha sheria ya kutaka rais ahudumu kwa mihula miwili pekee nchini humo
Mamlaka zimehamrisha kuzimwa kwa mitandao kwa muda wa siku mbili kama njia ya kukabiliana na maandamano hayo
No comments:
Post a Comment