chemical amtumbua stereo kua Ana mapenz ya dhati - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Wednesday, 6 September 2017

chemical amtumbua stereo kua Ana mapenz ya dhati


Image result for chemical picha 
Chemical.
RAPA wa kike anayefanya vizuri kwenye Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’, amefunguka kuwa, msanii Stereo ambaye amekuwa akijanasibu kwenye vyombo vya habari kwamba anampenda, ukweli ni kwamba mwanamuziki huyo hajawahi kumpenda
kwa dhati kwa kuwa bado mwanaume huyo hajamwonesha vitendo vyenye kuthibitisha hilo.
Stereo.
Akipiga stori na Showbiz Extra, Chemical alisema kuwa, hajawahi kupendwa kwa dhati na Stereo kwa kuwa hata siku moja, hajawahi kuelezwa kitu chochote kinachohusu mapenzi na rapa huyo, zaidi ya kumsikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Siwezi kujiongopea kwamba nimewahi kupendwa na Stereo, hata mara moja rapa huyo hajawahi kunipenda, nasema hivyo kwa sababu hajawahi kunifungukia live, ninaishia kumsikia tu kwenye media na mitandao ya kijamii,” alisema Chemical.

No comments:

Post a Comment