Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameahidi leo Septemba 11, 2017 kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki na kumfanyia maombi ili aweze kupona kwa haraka na kurudia katika hali yake ya zamani.
Gwajima amesema hayo leo alipokuwa kwenye kanisa lake la Ufufuo na uzima na kudai kwa wale ambao wanachukia au watakuwa hawajapenda kwa maamuzi hayo aliyofanya amewapa pole na kuwaambia atakwenda na kumuombea Mbunge huyo ili apone.
"Kesho mimi nitakwenda kumuona Tundu Lissu, nasema nitakwenda kumuona kama kuna kitu kinakuudhi shauri yako, nitakwenda na nitamuombea tena huko huko apone haraka na kurudi akiwa na nguvu zaidi, tumuombee mtu wa Mungu na mtu aliyerusha risasi kwa Lissu ajue kuwa zitarudi kwake pia" alisema Gwajima
Aidha Mchungaji Gwajima amesema kuwa huu si wakati wa kutoa lawama zozote kwa jeshi la polisi waachwe ili wafanya kazi yao na kudai kuwa wakiweza kuwapata au kutowapata hao waliofanya shambulio hilo basi watakuja kuongea baadaye.
"Mimi nilikuwa nje ya nchi kwa siku zaidi ya 80 hivyo mtandao wangu haujakaa sawa ila nasema hivi nitawajua, Kwenye hatua hii hatuwalaumu polisi, ila wakiwapata au kutompata hao watu hapo ndipo tutakuja kuogea baadaye" alisema Gwajima
Mbali na hilo Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Said Kubenea naye amesema kesho atakwenda nchini Kenya kwenda kumuoona Tundu Lissu na kusema licha ya kuwa ni mbunge mwenzake lakini pia ni rafiki yake wa karibu
No comments:
Post a Comment