Makombora ya Korea Kaskazini yanaweza kutungua ndege za abiria? - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 15 September 2017

Makombora ya Korea Kaskazini yanaweza kutungua ndege za abiria?

North Korean missile launch
Korea Kaskazini wanaporusha makombora kupitia anga ya Japan hadi kwenye bahari ya Pacific, makombora hayo hupitia anga ya kimataifa - juu ya eneo ambalo ndege za kubeba abiria na mizigo hupitia.
Ving'ora vilipolia Japan na kuwaonya raia watafute hifadhi, je, kuna uwezekano wa makombora ya Korea Kaskazini kugonga ndege iliyowabeba abiria?
Ni swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza kwani Pyongyang hurusha makombora yake bila kutoa tahadhari.
Uwezekano ni mdogo sana, lakini wataalamu wanasema kwamba ni jambo linaweza kutokea - kwamba kombora litungue ndege.
"Iwapo ndege ya abiria itagongwa na kombora, shinikizo za kuitaka Marekani na washirika wake wachukue hatua za kijeshi zitakuwa juu sana," anaonya Vipin Narang, profesa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Asia Kusini katika chuo kikuu cha teknolojia cha MIT.

Mambo yanavyoweza kwenda kombo

"Majaribio haya ya makombora yanaweza kuwa hatari kwa ndege za abiria na za mizigo," anakariri Ankit Panda, mhariri katika jarida la The Diplomat.
Korea Kaskazini huwa hawatangazi ni wakati gani watatekeleza makombora yao na yatapitia wapi.
Kawaida, nchi hutoa tahadhari kuhusu majaribio kama hayo na kufahamisha mashirika ya ndege pamoja na meli maeneo ambayo wanafaa kukwepa.
"Ni vigumu kupima hatari yenyewe hata hivyo," anasema Bw Panda. "Ni kiwango cha chini sana. Itakuwa ni kupima uwezekano wa vitu viwili vidogo kwa kiasi ukilinganisha na bahari au anga, vikikutana."

No comments:

Post a Comment