Wakati hali ya mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ikiwa bado haijatengemaa, yameibuka maswali kadhaa kuhusu shambulio dhidi yake lililotokea Alhamisi iliyopita mjini Dodoma.
Watu wasiojulikana walimshambulia rais huyo wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kwa risasi zipatazo 32 akiwa ndani ya gari lake baada ya kuwasili katika makazi yake eneo la Area D, na ni risasi tano zilizompata na kumjeruhi vibaya
Agosti 18, Lissu aliwaambia waandishi wa habari kuwa anafuatiliwa na watu anaowashuku kuwa ni maofisa usalama kwa takriban wiki tatu mfululizo.
Lissu, ambaye ameibukia kuwa mwanasiasa aasiyeogopa kusema analoamini, amelazwa Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi ambako amewekwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu.
Taarifa zilizopatikana jana zinasema mbunge huyo, bado anaangaliwa kwa karibu na madaktari.
Habari za shambulio dhidi yake zilitapakaa kwa kasi Ijumaa mchana, na juzi watu walikuwa wakitoa salamu za pole na kumuombea arudi katika hali yake, lakini jana kukaibuka maswali.
Gazeti hili limeyachambua maswali machache kati ya mengi ambayo yamejitokeza katika mijadala mbalimbali.
Miongoni mwa maswali hayo ni kwa nini Jeshi la Polisi halikuchukua hatua baada ya Lissu kutangaza kuwa kuna watu wanamfuatilia kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment