Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge
wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge
ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu
Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.
Pia Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT
Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na
Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti
Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili
fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya
risasi alizopigwa Lissu.
No comments:
Post a Comment