MKONGWE asiyechuja kwenye Hip Hop Bongo ambaye pia ni msomi wa Shahada ya Uzamivu (Master Degree), Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amefunguka kuwa, katika historia ya maisha yake, aliwahi kuwa wa mwisho katika mitihani ya kishule alipokuwa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kigoma.
Akipiga stori na Showbiz Extra, Nikki alisema kuwa, ingawa imepita miaka mingi, lakini kamwe hawezi kusahau siku ambayo ‘alishika mkia’ katika mtihani wa katikati ya mhula akiwa kidato cha kwanza.
“Nilikuwa wa mwisho kwenye matokeo ya mwezi wa sita nikiwa kidato cha kwanza, kwa kweli siwezi kusahau, ukweli ni kwamba jambo hilo lilisabababishwa na kuchelewa kuripoti kwa wakati baada tu ya matokeo ya darasa la saba. Baada ya kuripoti, wiki chache baadaye, nikakutana na mtihani, nikazungusha yai la maana,” alisema Nikki
No comments:
Post a Comment