nilikimbiwa na msanii mwenzangu hotelini asema amber lulu - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 22 September 2017

nilikimbiwa na msanii mwenzangu hotelini asema amber lulu

 Image result for Amber Lulu

MSANII na mnenguaji  wa kwenye video za wasanii (video vixen) Amber Lulu, ambaye  anatamba na wimbo wake wa Only You amefunguka kuhusu kukimbiwa hotelini na aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza tangu anafika Dar es salaam, mwigizaji Rammy Galis, bila sababu.

Alipoulizwa juu ya  stori hiyo, Amber Lulu alifunguka na kusema:
“Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa Rammy Galis kipindi nafika Dar, tulikubaliana vizuri na Rammy tukaenda hotelini tukaagiza vyakula tukala na mambo mengine yakaendelea. Baadaye akaniambia nakuja, nikamwambia poa lakini mwisho wa siku sikumuona.  Nikawa napiga simu yake mara asipokee na akipokea basi akawa ananiambia nisubiri kidogo.  Sikujua kwa nini alikuwa anafanya hivyo.”

Aliongeza kwamba: “Alinipokea mizigo vizuri tukaingia hotelini baada ya hapo ndo akafanya alivyoamua kufanya, basi mimi nikampigia dad’angu simu nikamuelezea akaniambia hayo ni mambo ya kawaida basi dada  akanitumia pesa nikalipia kila kitu. Baada ya hapo nikarudi zangu nyumbani na sikuwahi kuwasiliana naye tena  tangu siku hiyo. “

Amber ni mwanamke asiyeishiwa kiki na skendo mjini lakini hajalikitu, anaangalia maisha yake tu.  Ni msichana ambaye haogopi kufunguka mambo yanayohusiana na mahusiano yake.  Haogopi kiki bali anazipenda kiki.

No comments:

Post a Comment