Pia Young Killer alisema kuwa mashabiki wasimfananishe na hao watu kwani haendani nao hata kidogo.
Alichofunguka Young Dee kuhusu kauli ya Young Killer kusema hawamuwezi, ni kuwa Young Killer na Dogo Janja ni vifaranga vyake, kwa hiyo hawamuwezi hata kidogo.
Alipoulizwa kama ikitokea shoo ya pamoja baina ya yeye, Dogo Janja na Young Killer, alisema uwezo wake ni mkubwa sana, hawezi kufanya shoo kwenye jukwaa moja nao.
”Inategemea hiyo shoo imeandaliwa kwa aina gani kwa sababu mimi sasa hivi nimekua, kwa hiyo siwezi kufanya shoo ya pamoja na hao vifaranga vyangu. Sidhani kama itakuwa shoo nzuri kwa mashabiki zangu kwa sababu mimi nikiwa jukwani ni mtu mkubwa sana. Ukiwakusanya wote hao labda ndiyo unaweza kupata nusu ya Young Dee,” alisema Young Dee
Siku zote hamna msanii ambaye anakubali kufunikwa lakini hii ya hawa vijana wanaofanya muziki wa HipHop imekuwa balaa pale kila mtu anapojiona yupo juu ya mwenziye, lakini wote ni wakali wa HipHop kutoka Tanzania kwenye kisiwa cha burudani.
No comments:
Post a Comment