MBUNGE wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa
amefunguka na kusema kuwa amepata taarifa jeshi la polisi linamtafuta
na kusema endapo jeshi hilo litamuita kwa kufuata utaratibu basi
ataitika wito huo ila si kuviziwa
Msigwa ametoa taarifa hiyo kufuatia
kuwepo kwa taarifa toka jana kuwa kiongozi huyo anatafutwa na jeshi hilo
akidaiwa kuwa ni mmoja kati ya waliokuwa wakiratibu mkusanyiko ambao
ulitakiwa kufanyika jana kumuombea Mbunge Tundu Lissu katika Viwanja vya
TIP Sinza, jambo ambalo amepinga na kusema bado yupo nchini Kenya.
“Nimepata taarifa kuwa polisi
wamenitafuta toka asubuhi (jana) maeneo ya Sinza, wakisisitiza kuwa nipo
hotelini hapo, wakati mimi niko Nairobi.
“Nitaitika wito wa polisi ukiletwa rasmi, sihitaji kuviziwa, +255754360996 mnaweza kunipigia au kunitumia ujumbe mfupi WhatsApp,” alisema Msigwa.
Mbunge huyo bado yupo jijini Nairobi
kwenye matibabu ya Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment